Na Renalda Mwarabu
|
Mwalimu mlezi wa wanafunzi
Bwana Nestory Ihano akizungumza na wanafunzi kwa habari ya kujali na
kutunza muda. (Picha na Nickson Mafuru)
|
Mwalimu mlezi wa wanafunzi ambaye pia ni mkuu wa kitengo
cha uongozi na usimamizi katika chuo cha Habari Maalum, ndugu Nestory Ihano,
amewataka wanafunzi kuzingatia na kutunza matumizi ya muda, pindi wanapokuwa
chuoni, hali ambayo itawapelekea kuwa watendaji wazuri baadaye.
Amesema hayo wakati akitoa matangazo ya kila siku katika
chumba cha mikutano, mara baada ya kumaliza maombi ya asubuhi, na kusema kuwa
tatizo la uchelewaji ni tatizo ambalo
linataka kuwa sugu kwa baadhi ya wanafunzi, na kwamba hali hiyo itapelekea
maisha ya baadhi ya wanafunzi kuwa magumu siku za mbeleni kwani muda ndiyo uti wa mgongo wa maendeleo.
Bwana Ihano amewaasa wanafunzi kufuata sheria za chuo ikiwa
ni pamoja na kujali muda wa vipindi, na kujifunza kufanya mambo kwa wakati
husika, kwani baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakipuuzia kuhudhulia maombi ya
asubuhi ambapo ni moja kati ya taratibu za chuo.
Naye mmoja wa waalimu wa chuo hicho, Mwalimu Emmy Kimaro, ambaye
ni mwalimu wa masomo ya Public Relation and Advertising, Media Law, pamoja na
somo la Studying techniques, amesema wanafunzi wanayo nidhamu, lakini ipo
changamoto ya matumizi ya muda wa darasani, ambapo wanafunzi wamekuwa
wakichelewa madarasani na kuwakuta waalimu wakiwepo tayari darasani, hali ambayo
haitakiwi kitaaluma, kwani hupelekea kupoteza
umakini wa wanafunzi wanapokuwa madarasani.
|
Mwalimu Emmy Kimaro
akizungumzia changamoto zilizopo katika suala Zima la nidhamu ya muda
chuoni Habari Maalum. (Picha na Asaph Bimila).
|
Mwalimu Emmy ameongeza kwa kusema kuwa, changamoto
nyingine inatokea pale ambapo wanafunzi
wanaposhindwa kufika chuoni asubuhi kwa muda uliopangwa kwaajili ya maombi ya
asubuhi .
Ametoa wito kwa wanafunzi wote kuwa, wanatakiwa kutumia muda
walionao vizuri, kwani muda huwa haujirudii na kuhakikisha wanafanya kila jambo
kwa wakati husika ili kufikia malengo yao.
Mmoja wa wanafunzi wa chuo cha Habari Maalum, Adelphina Pius,
amezitaja baadhi ya sababu zinazompelekea mwanafunzi kutokuheshimu muda, kuwa ni
pamoja na uvivu ,kuto kuutambua wajibu na malengo, lakini pia kutokujali
umuhimu wa elimu, na kupelekea wanafunzi
kuto fanikiwa kwa viwango vinavyotakiwa.
Kwa upande wake Makamo mkuu wa chuo taaluma, Bwana Lazarus
Laizer, amesema nidhamu Ya utunzaji wa muda kwa wanafunzi, inaridhisha kwani
amekuwa akifanya uchunguzi wa kina juu ya wanafunzi na kuona kwamba wanafunzi wanajitahidi
kujishughulisha katika nyanja mbalimbali za masomo muda wote wanapokuwepo
chuoni.
Lazarus amesema ,
siku za nyuma wanafunzi walikuwa wakizagaa hovyo na kuhakiki kuwa ni jambo
la tofaauti sana, kuona kwamba katika muhula huu nidhamu ya matumizi ya muda
imeimarika tofauti na siku za nyuma.
|
Makamo Mkuu wa Chuo Taaluma Bwana
Lazarus Laizer akizungumzia mwenendo wa nidhamu ya muda
kitaaluma chuoni Habari Maalum ( Picha na Asaph Bimila).
|
Aidha, Lazarus amesema bado kuna changamoto kubwa kwa baadhi
ya wanafunzi, kwani wanachelewa kufika asubuhi katika muda wa maombi kwa kuzingatia kwamba, chuo
kimejenga misingi yake juu ya maombi na hivyo kila mwafunzi anatakiwa
kujihusisha katika suala zima la maombi lakini baadhi yao wamekuwa wakilipuuzia
hilio.
Lazarus ametoa wito kwa wanafunzi wote kuwa wanatakiwa
kufuata utamaduni wa chuo, kwani kila mahali kuna tamaduni na sheria ambazo ni
lazima kila mtu aishi akiongozwa nazo.