Jumuiya mbalimbali zisizo za serikali (NGO's) zimetoa wito wa
kufanyika uchunguzi kuhusu mauaji ya wanakijiji huko mashariki mwa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Innocent Segihobe ambaye ni Katibu Mkuu wa jumuiya zisizo za serikali amesema uchunguzi huo unapaswa kuweka wazi majukumu ya kufanya baada ya mauaji ya wanakijiji cha Nyanzale katika eneo la Rusthuru huko Kivu Kaskazini, Congo DR. Segihobe amewatuhumu viongozi wa kisiasa wa eneo la Rusthuru kwamba wanahusika katika kudumisha machafuko na mapigano huko Kivu Kaskazini.
Mapigano yaliyotokea baina ya wakimbizi na wakazi wa kijiji cha Rusthuru yalianza baada ya kupatikana maiti ya mkimbizi mmoja katika eneo hilo.
Wakimbizi hao wanawatuhumu wanakijiji kuwa ndio waliomuua mkimbizi mwenzao.
Watu watano wameripotiwa kuuawa na nyumba zaidi ya 40 kuteketezwa kwa moto katika machafuko hayo.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Rusthuru wamekimbilia katika kambi za askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.
Chanzo radio Terhan
facinatting
ReplyDelete