Na Renalda Mwarabu
Umoja wa waendesha Bodaboda Mkoa
wa Mwanza kwa paamoja wamekubaliana kwa sauti moja kuanzishwa kwa Umoja
wa Bodaboda Taifa ili kurahisisha utatuzi wa Changamoto zinazoikabiri
sekta ya usafirishaji abiria ya kwa njia hiyo ya Bodaboda.
Kufuatia
mkutano wao Mkuu wa mwaka ambao mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya
Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga (pichani) ambae alimwakilisha
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Katika Mkutano
huo, Konisaga ambae alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, alitaka jeshi
la polisi kitengo cha usalama barabara kuzidisha juhudi za kutoa elimu
ya usalama barabarani ili kupunguza ajali, badala ya kasi iliyopo ya
kutoza faini kwa watumiaji wa vyombo vya barabarani.
Mwenyekiti wa
bodaboda Mkoa wa Mwanza Makoye Kayanda amesema "pamoja na Mambo
mengine, Wajumbe wa Mkutano huo walikubaliana kwa sauti moja kuanzishwa
kwa Umoja wa Bodaboda Taifa ili kurahisisha utatuzi wa Changamoto
zinazoikabiri sekta ya usafirishaji abiria ya Bodaboda".
Amesema miongoni
mwa changamoto hizo ni pamoja na kuvamiwa, kutekwa, kuuawa na kuuawa kwa
waendesha bodaboda huku bodaboda zao zikiibiwa. Kutafuta suluhu ya
baadhi ya watu wakiwemo bodaboda kutumia fursa hiyo katika kujihusisha
na uhalifu nchini.
Utii wa Sheria bila shuruti pamoja na kujadili namna
bodaboda wanavyoweza kushirikiana na taasisi mbalimbali zikiwemo za
binafsi na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya sekta hiyo.
Mkutano huo
ulihudhuriwa na Viongozi wengine wa Bodaboda kutoka Mikoa ya Mara,
Tabora, Singida, Shinyanga, Kilimanjaro pamoja na Viongozi wa sekta
nyingine ambazo ni wadau wa usafirishaji ambao ni Machinga, Mamalishe,
Daladala, Mabasi, RTO, Sumatra pamoja na TRA. Chanzo Mo blog