Mahakama
ya Hakimu Mkazi mjini Singida, imewahukumu majangili saba adhabu ya
kutumikia jela ya miaka 140 na kulipa faini ya zaidi ya shilingi 1.9
bilioni baada ya kuwatia hatiani kwa kwa makosa 12 likiemo la kumiliki
bunduki ya kijeshi SMG waliyokuwa wanaitumia kuulia Tembo.
Baadhi
ya makosa mengine ni kuunda umoja /ushirikiano wa kufanya uhalifu wa
kuuawa wanyapori wakiwemo Tembo, kufanya biashara haramu ya kuuza nyara
za serikali na kumiliki meno ya Tembo bila kwa na kibali.
Washitakiwa
hao ambao kesi yao ilipewa namba 5/2015, ni Yusuph Masala Jidavi (39)
mkulima kijiji cha Yongo Manda mkoani Katavi, Elias John Sprian (30)
mkazi wa Kijiji cha Ng’ambe mkoani Tabora na Salum Mohammed Ngasa (31)
mkazi wa kijiji cha Imalampaka Sasilo wilaya ya Manyoni.
Wengine
ni Yona Stanley @Yohana (26) mkazi wa kijiji cha Mbwasa Sasilo wilaya
ya Manyoni, Ramadhani Salum Hatibu (33) mkulima kijiji cha Mgulu wa
Ng’ambe wilaya ya Manyoni,Kulwa Saidi Salum (28) mkulima kijiji cha
Sikonge mkoani Tabora na Buhoro Salehe Lubaha Yakonie (37)@ Buhoro
mkazi wa Kambi ya Wakimbizi Katumba mkoani Tabora.
Mwendesha
mashtaka na mwanasheria wa serikali Pretrida Mutta, alidai mbele ya
Hakimu mfawidhi mwandamizi na mahakama hiyo, Joyce Minde, kuwa kati ya
Agosti mwaka 2013 na Julai nane mwaka 2014, washitakiwa kwa pamoja
walikamatwa wakimiliki vipande 28 vya meno ya Tembo vyenye thamani zaidi
ya shilling 34.1 milioni.
Mutta
alisema pia washitakiwa hao walikamatwa wakimiliki kinyume na sheria
‘Elephant tufts’ sita zenye thamani ya shilingi 192 milioni, kipande cha
ngozi ya Simba chenye thamani ya zaidi ya shilingi 7.8 milioni na ngozi
ya kudu ya shilingi 3.5 milioni.
Kabla
ya kutolewa kwa hukumu, Mwanasheria wa serikali Mutta, aliiomba
mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa washitakiwa, ili iwe fundisho kwao
na kuogofya watu wengine wanaotarajia kujihusisha biashara haramu ya
kuuza nyara za serikali.
Kwa
upande wa washitakiwa ambao wakili wao na kujitegemea Josephat Wawa
ambaye hakuwepo Mahakamani, washitakiwa kila mmoja kwa wakati wake,
aliiomba mahaka hiyo impe adhabu nafuu kwa madai mbalimbali likiwemola
kutegemewa na familia.
Akitoa
hukumu hiyo, Hakimu Minde, alisema kuwa upande wa mashitaka
umethibitisha bila kuacha chembe chembe ya shaka kwa hali hiyo
washitakiwa wana hatia kama walivyoshitakiwa.
“Kila
mshitakiwa atatumikia jela miaka 20 na kulipa faini ya zaidi ya
shilingi 274.2 milioni adhabu hizi ni fundisho kwenu na pia kuwaogofya
watu wengine wanaotarajia kutenda makosa ya aina hii”,alisema Hakimu
Minde.Chanzo Radio Terhan.
No comments:
Post a Comment