Kamishna Mkuu wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa maelfu ya Warundi wamekimbilia katika nchi jirani.
Msemaji wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa, Melissa Fleming amesema kuwa, tangu Aprili mwaka 2015 hadi sasa wakimbizi laki tano na 946 wa Burundi wamekimbilia katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Tanzania, Rwanda, Uganda na Zambia.
Melissa Fleming ameongeza kuwa hadi sasa hakujapatikana maendeleo ya maana katika uwanja wa haki za binadamu na usalama wa ndani nchini Burundi licha ya juhudi zote zilizofanyika na kwamba hali mbaya ya uchumi yumkini ikazidisha idadi ya wakimbizi katika siku za usoni.
Machafuko ya ndani nchini Burundi yalianza baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kuwania tena kiti hicho kwa mara ya tatu mfulilizo. Wapinzani wanasema hatua hiyo ilikiuka katiba ya nchi na makubaliano ya amani ya Arusha yaliyohitimisha vita vya ndani.(Chanzo Radio Terhan)
No comments:
Post a Comment