Saturday, 26 March 2016

Bodaboda Mkoani Mwanza wataka kuanzishwa kwa Umoja wa Kitaifa wa Bodaboda


 Na Renalda Mwarabu

 
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu) akuzungumza katika Mkutano Mkuu Muhula wa Kwanza wa mwaka 2016 wa Umoja wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Mwanza uliofanyika Jumamosi Machi 19,2016 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Pamba Jijini Mwanza. Kushoto kwake ni viongozi wa bodaboda Mkoa wa Mwanza.


Umoja wa waendesha Bodaboda Mkoa wa Mwanza  kwa paamoja wamekubaliana kwa sauti moja kuanzishwa kwa Umoja wa Bodaboda Taifa ili kurahisisha utatuzi wa Changamoto zinazoikabiri sekta ya usafirishaji abiria ya  kwa njia hiyo ya Bodaboda.
Kufuatia mkutano wao Mkuu wa mwaka ambao mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga (pichani) ambae alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Katika Mkutano huo, Konisaga ambae alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, alitaka jeshi la polisi kitengo cha usalama barabara kuzidisha juhudi za kutoa elimu ya usalama barabarani ili kupunguza ajali, badala ya kasi iliyopo ya kutoza faini kwa watumiaji wa vyombo vya barabarani.

Mwenyekiti wa bodaboda Mkoa wa Mwanza Makoye  Kayanda amesema "pamoja na Mambo mengine, Wajumbe wa Mkutano huo walikubaliana kwa sauti moja kuanzishwa kwa Umoja wa Bodaboda Taifa ili kurahisisha utatuzi wa Changamoto zinazoikabiri sekta ya usafirishaji abiria ya Bodaboda".

Amesema miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na kuvamiwa, kutekwa, kuuawa na kuuawa kwa waendesha bodaboda huku bodaboda zao zikiibiwa. Kutafuta suluhu ya baadhi ya watu wakiwemo bodaboda kutumia fursa hiyo katika kujihusisha na uhalifu nchini. 
 
Utii wa Sheria bila shuruti pamoja na kujadili namna bodaboda wanavyoweza kushirikiana na taasisi mbalimbali zikiwemo za binafsi na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya sekta hiyo.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Viongozi wengine wa Bodaboda kutoka Mikoa ya Mara, Tabora, Singida, Shinyanga, Kilimanjaro pamoja na Viongozi wa sekta nyingine ambazo ni wadau wa usafirishaji ambao ni Machinga, Mamalishe, Daladala, Mabasi, RTO, Sumatra pamoja na TRA. Chanzo Mo blog

No comments:

Post a Comment