Na Renalda Mwarabu
Jumuiya ya Afrika Mashariki ,EAC, inakaribia kuunda jeshi la
pamoja kwa lengo la kulinda taasisi muhimu za kiuchumi za nchi
wanachama.
Hayo yamebainika wakati wa mafunzo ya pamoja mjini Nairobi ya wanajeshi 300 kutoka Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi na Rwanda.
Kamanda wa Majeshi ya Kenya Jenerali Samson Mwathethe amesema kikosi
hicho cha pamoja ni muhimu kwa kuzingatia matarajio makubwa ya ustawi wa
kiuchumi Uganda na Kenya kutokana na uzalishaji mafuta na gesi asilia
Tanzania.
Akizungumza Ijumaa wakati wa mazoezi hayo Jenerali Mwatheteh amesema,
“Shirikisho limeanza kupata muundo wake hatua kwa hatua kama
ilivyopangwa na nchi zote za EAC ikiwemo Sudan Kusini. Eneo hili lina
ukubwa wa mita mraba milioni 2.4 na idadi ya watu milioni 170.
Nchi zote
wanachama zinafungamana na udumishwaji amani na usalama katika eneo.”
Mkuu wa Jeshi la Kenya amesema ugaidi ni tishio kubwa zaidi la
usalama katika eneo na hivyo nchi zote zinapaswa kushirikiana.
Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Ulinzi wa Kenya
Raychelle Omamo
amesema mafunzo hayo ya maafisa wa kijeshi ni katika fremu ya
ushirikiano wa kiulinzi baina ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha amesema vikosi vya usalama vinapaswa kufahami mbinu za makundi ya
kigaidi yanayolenga kuvuruga uchumi wa eneo hilo. Chanzo radio Terhan
No comments:
Post a Comment